Wakulima wa zao la Pareto nchini Kenya wameanza kuona faida ya kilimo hicho. Maua hayo hukaushwa mara baada tu ya kuyachuma. Maua hayo husagwa kiwandani ili kupata sumu aina ya "pyrethrin" ambayo hutumika kwa ajili ya kutengeneza dawa ya kuua wadudu waharibifu.