DW imechagua Kiswahili kama lugha ya mawasiliano
Wrong language? Change it here.

Matukio ya Kisiasa

Operesheni kupambana na waasi yaanza Ukraine

ImageOperesheni iliokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ya kuwan'gowa wanaharakati wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine imeanza wakati Urusi ikitupilia mbali madai kwamba imeweka vikosi vyake katika eneo hilo.

Matukio ya Kisiasa

Syria yakabidhi asilimia 65 ya silaha za kemikali

Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Silaha za Atomiki, OPCW, wamesema wanatiwa wasiwasi na kasi ya Syria katika kukabidhi silaha zake za atomiki.

Matukio ya Kisiasa

Hali inatisha Ukraine : Muda wa kuweka chini Silaha Umemalizika

Kitisho cha kuripuka vita vya wenyewe kwa wenyewe kinazidi kukua nchini Ukraine.Urusi inatuhumiwa na nchi za magharibi kuwakusanya maelfu ya wanajeshi karibu na mpaka wa mashariki wa nchi hiyo

Matukio ya Kisiasa

Matumizi ya kijeshi yapungua duniani

Matumizi ya kijeshi duniani yamepungua katika mwaka wa 2013 kutokana na kupungua kwa matumizi nchini Marekani na katika mataifa mengine ya magharibi, lakini matumizi katika mataifa yanayoinukia kiuchumi yameongezeka.

Matukio ya Afrika

Wakimbizi wa Sudan Kusini watiririka Ethiopia

Takribani wakimbizi 1000 kutoka Sudan Kusini huingia nchini Ethiopia kila siku, wengi wao wakiwa katika hali mahtuti. Haya yameelezwa na Umoja wa Mataifa, ambao pia umesema 95% ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto.

Matukio ya Afrika

Mripuko wauwa 71 Abuja

Mripuko wa bomu wakati wa harakati za asubuhi kwenye kituo cha basi katika kiunga cha mji mkuu wa Nigeria Abuja umeuwa takriban watu 71 Jumatatu (14.04.2014) na kuzusha wasi wasi juu ya kuenea kwa uasi wa Boko Haram.

Matukio ya Afrika

Watoto wa Gaddafi kusimamishwa kizimbani

Wana wawili wa kiongozi wa zamani wa Libya Muamar Gaddafi wanafikishwa mahakamani leo, katika kesi ambayo vile vile inawahusisha maafisa wengine wapatao 30 wa enzi za utawala wa Gaddafi.

Matukio ya Afrika

Hatimae uchaguzi wafanyika Guinea-Bissau

Hakuna uchaguzi barani Afrika uliokuwa ukisitishwa na kuahirishwa mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni kama ule wa Guinea-Bissau.Hatimae unafanyika Jumapili (13.04.2014) kumchaguwa rais na bunge.

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya Ukraine

Wahariri wa magazeti wanazungumzia juu ya mgogoro wa Ukraine na juu ya biashara ya silaha kati ya Ujerumani na Saudi Arabia

Michezo

Mo Farah ashindwa kung'ara katika marathon

Alijiunga na magwiji wenzake kwa mazoezi ya wiki mbili katika maeneo ya nyanda za juu nchini Kenya, na wengi walisubiri kuona kama angeupita mtihani wa kukimbia mbio za marathon kwa mara ya kwanza maishani mwake.

Masuala ya Jamii

Muuguzi ashtakiwa Uganda kwa kueneza UKIMWI

Muuguzi wa kike mwenye umri wa miaka 64, Rosemary Namubiru amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kuuwa, amenyinwa dhamana na kupelekwa gerezani katika kesi kama mfano wa kuwepo kanuni za kizembe hospitalini nchini Uganda.

Matukio ya Afrika

Umoja wa Mataifa na hali ya usalama nchini Burundi

Umoja wa mataifa umeitahadharisha serikali ya Burundi na kuitaka kuchukua hatua zinazohitajika ili kukabiliana na kuzidi kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiusalama.